Na Byarugaba Innocent, Kibaha
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeiwezesha halmashauri ya Mji Kibaha kuendelea na jitihada za kujenga na kuboresha miundombinu ya utoaji wa elimu kwenye shule za Msingi baada ya kuidhinisha shilingi 813,537,908.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amemshukuru Mhe.Samia Suhuhu Hassan kwa kuidhinisha kiwango hicho cha fedha ili kitumike kuboresha miundombinu ya shule za Msingi huku akitoa wito kwa wadau wote kuilinda ili idumu kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Ofisa Elimu Msingi Bernadina Kahabuka,imetaja miundombinu inayojengwa kuwa ni vyumba vya madarasa,ukarabati wa vyumba vilivyochakaa,ujenzi wa nyumba za walimu,ununuzi wa madawati na ukarabati wa madawati chakavu, ujenzi wa matundu ya vyoo,ujenzi wa gata za kuvunia Maji na uchimbaji wa kisima. (3).jpeg
Kahabuka ameongeza kuwa kiasi cha milioni 310,000,000 kimetoka kwenye Mapato ya ndani ya halmashauri, Serikali kuu imetoa milioni 51,250,000 huku mpango wa kukabiliana na UVIKO-19 kwa fedha iliyokopwa IMF kwa masharti nafuu ukichangia milioni 108,882,379.
Aidha,wadau wa Maji RUWASA,wamechangia milioni 15,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa choo kata ya Pangani huku mpango wa kulipa kulingana na Matokeo (EP4R) ukichangia milioni 328,405,529.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Msingi Tumbi Saimon Minja ameeleza kuwa uimarishaji na Uboreshaji wa miundombinu umekuwa wa tija shuleni hapo kwani umechochea mahudhurio ya wanafunzi, Wazazi wameongeza Kasi ya uandikishaji kutokana na Mazingira ya shule kuwa ya kuvutia.
Halmashauri ya Mji Kibaha jumla ya shule za Msingi 44.
Haki Zote Zimahifadhiwa