STENDI KUU MPYA KIBAHA KUANZA KUTUMIKA RASMI TAREHE 01/10/2018.
Mkurugenzi wa Mji Kibaha bi. Jenifa Omolo amesema kuwa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani kitaanza rasmi kutumika Jumatatu tarehe 01/10/2018 kwani ujenzi wake umekamilika. Stendi hii pamoja na jengo la utawala vimegharimu zaidi ya Tsh.billion 3.3 huku ikiwa na uwezo wa kuingiza mabasi makubwa 24, Mabasi ya kati 48 huku magari mengine 60 na tax yakiegeshwa kwa wakati mmoja. Aidha, Miundombinu mingine iliyopo ni kituo cha polisi, vyoo, Kizimba cha taka, sehemu ya kupumzikia wasafiri, Mghahawa, Taa za usiku huku kituo kikizungushiwa uzio maridadi uliopambwa kwa bustani inayovutia. Mustapha Issa (muwakilishi wa mawakala wa Mabasi makubwa yaendayo Mkoani) amekiri kufurahishwa na ujenzi huo huku akimpongeza Mkurugenzi kwa kutatua kero ya muda mrefu ya stendi inayotumika sasa kuwa ni finyu na hujaa tope wakati wa mvua.
Haki Zote Zimahifadhiwa