HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA KIBAHA MHE. ASSUMPTER MSHAMA KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI PIKIPIKI KWA MAOFISA ELIMU KATA, ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA MAILIMOJA, TAREHE 13/08/2018
Ndugu;
Nina furaha kusimama mbele yenu nikiwa Mkuu wenu wa wilaya ya Kibaha kutoa pongezi kubwa kwa kazi mnazofanya katika kuendeleza gurudumu la maendeleo ikiwemo Elimu katika nchi yetu ya Tanzania.
Nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anazozifanya kwa kuhakikisha Elimu bila malipo inafika katika maeneo yote ya Tanzania.
Ndugu wananchi; Halmashauri ya Mji Kibaha Ina jumla ya shule za Msingi 57 na Sekondari 36. Aidha shule za Msingi za Serikali 39 na 18 za binafsi. Pia shule za Sekondari za Serikali ni 13 na binafsi 23.
Uandikishaji kwa shule za awali na darasa la kwanza (STD I) umekua ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mwaka huu 2018 idadi ya wanafunzi wa awali Imeongezeka kutoka 3127 hadi kufikia 3176 sawa na 101% na kwa darasa la kwanza imeongezeka kutoka 4734 hadi kufikia wanafunzi 5106 sawa na 116% kwa shule za serikali.
Vilevile ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba umekua ukiongezeka mwaka hadi mwaka, mfano mwaka 2016 wanafunzi waliosajiliwa kuingia kidato cha kwanza walikua 2271 sawa na asilimia 76.28%, na mwaka 2017 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza walikuwa 2608 ambapo wavulana 1331 na wasichana 1277, walioripoti wavulana 1130, wasichana 1172 jumla ni 2302 ni sawa na asilimia 88, hivyo kuingia kidato cha kwanza mwaka 2018.
Ndugu wananchi; Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuikabili Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. Sekta ya Elimuu na mafunzo kwa mujibu wa Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 na mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika. Hivyo basi serikali yetu ya awamu ya tano kwa usimamizi wa jemedari wetu Mh. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kupitia mradi wa LANES (Literacy Arithmetic and Numecracy Education Support) imewezeshaa kutoa mafunzo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa walimu wa darasa la I na II ili waweze kufundisha madarasa hayo kwa umahiri, kufadhili vituo 10 vya MEMKWA katika kila Wilaya na kuwezesha mafunzo kwa kamati za shule ili ziweze kusimamia na kuendesha shughuli za kielimu kwa weledi mkubwa.
Ndugu wananchi; Kubwa zaidi ni kutoa vitendea kazi yaani pikipiki kwa Waratibu Elimu Kata ili kurahisisha usimamizi na ufuatiliaji kwa umahiri shughuli za kielimu za ujifunzaji na ufundishaji katika maeneo yao ya kazi.
Kipekee kabisa, Nimshukuru tena Mh. Raisi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwezesha kupatikana pikipiki hizi ambazo leo hii mimi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, nawakabidhi ninyi waratibu elimu kata wangu wa Halmashauri ya Mji Kibaha pikipiki hizi kuwezakutekeleza majukumu yenu kwa weledi.
Nipende kuwakumbusha majukumu yenu kwa uchache ili muweze kuyatekeleza kwa ukamilifu. Majukumu hayo ni pamoja na:
Ni matumaini yangu kuwa mmesoma vyema mkataba/ mikataba mliyopewa na Mkurugenzi wenu inayoelekeza juu ya matumizi sahihi ya pikipiki mtakazo kabidhiwa leo hii.
Ndugu wananchi; Kuna changamoto ambayo inalazimu leo hii nijadili kwa kina pamoja nanyi. Changamoto hiyo ni UTORO wa wanafunzi wa shule zetu unaosababisha kutofanya mitihani ya kitaifa ya Elimu ya msingi na sekondari. Changamoto hii inapelekea kushusha ufaulu kwa ufaulu kwa Wilaya yetu.
AGIZO:
Ninawaagiza wananchi wote na watendaji wote katika kila sekta, kuhakikisha kwamba watoto wote walioandikishwa katika nyanja tofautitofauti za elimu wanahudhuria shuleni na kufanya mitihani yao yote ya ndani nay a kitaifa bila kuishia njiani.
Ninawashukuru wote kwa utulivu na kunisikiliza, ahsanteni sana.
SERIKALI YA CCM HOYEEEEEEEEEEEEEEEE,
ELIMU SAAAFIIIII, .
Assumpter Mshama,
MKUU WA WILAYA,
KIBAHA
Haki Zote Zimahifadhiwa