• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Waganga wakuu Tanzania wamtunuku Rais Samia Suluhu Hassan Tuzo, Dkt Mpango atoa maagizo.

Posted on: July 12th, 2025



Na John Mapepele


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo.


Tuzo hiyo ameitoa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamo wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.

Mbali na tuzo hiyo pia Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama.


Mhe. Mpango  amewapongeza Waganga Wakuu nchini

kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia  wananchi huku akiwataka waendelee

kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao.


Amesisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana hali halisi ya uchumi.


"Nawaelekeza Mawaziri wa Afya na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha washughulikie suala la ucheleweshaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya." Amesisitiza Mhe. Mpango


Amesema kwa sasa Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa  kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.


Pia amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri/Manispaa na Majiji kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ya afya na vifaa tiba katika Halmashauri/Manispaa/Majiji.


Amesema ili kuimarisha huduma za afya na usimamizi shirikishi, Serikali imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na  mashine za kisasa za kidijiti (Digital X-ray na ultrasound) na kuagiza kuvitunza vifaa hivyo na vingine vitakavyonunuliwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.


Akimkaribisha Mhe. Mpango kutoa hotuba, Mhe.Mchengerwa amemshukuru Rais Samia kwa maono yake makubwa na miongozo kwenye sekta ya afya ambayo yameleta mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi.


Mhe. Mchengerwa ametumia mkutano huo kutaja mafanikio lukuki yaliyopatikana katika kipindi hiki.


Aidha, amesema  mafanikio hayo pia yanatokana na ushirikiano baina ya Wizara yake na Wizara ya Afya.


Katika mkutano huo wadau mbalimbali ya afya pia wametunukiwa vyeti vya kutambua michango yao.

Matangazo

  • INEC yahimiza Wananchi mikoa 16 kujitokeza uboreshaji Daftari awamu ya pili May 14, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Waganga wakuu Tanzania wamtunuku Rais Samia Suluhu Hassan Tuzo, Dkt Mpango atoa maagizo.

    July 12, 2025
  • Wananchi Manspaa ya Kibaha kunufaika na Huduma Bora, baada ya mji kupandishwa hadhi ya kuwa manspaa

    July 12, 2025
  • Mkurugenzi Manspaa ya Kibaha Dkt Rogers Shemwelekwa awataka Wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara Manspaa ya Kibaha

    July 10, 2025
  • WATENDAJI wa Kata Manspaa ya Kibaha watembelea Halmashauri ya Mji Tunduma

    July 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

Watendaji wa Kata Manspaa ya Kibaha waibua mazito mafunzo mbeya
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa