Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kuipatia Halmashauri ya Mji Kibaha kiasi cha fedha shilingi 760 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha Kwanza,2023 kesho Oktoba 5,2022 jumla ya wanafunzi 5145 wanaketi kuanza kufanya Mtihani wa Taifa kuhitimisha safari yao ya miaka Saba shule ya Msingi.
Afisa Elimu taaluma wa Halmashauri ya Mji Kibaha Agatha Komba amethibitisha na kwamba maandalizi kwenye shule zote 61 zenye watahiniwa maandalizi yamekamilika huku jumla ya mikondo 229 ukiwemo mkondo mmoja kwa ajili ya mwanafunzi mwenye mahitaji maalum
Aidha,Komba ameeleza kuwa miongoni mwa watakaofanya Mtihani huo wapo wavulana 2527 sawa na asilimia 49.1 huku wasichana wakiwa 2618 sawa na asilimia 50.9
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema hana shaka na maandalizi ya wanafunzi wenyewe kwani walimu wamewafundisha kikamilifu hivyo wakatumie maarifa waliyoyapata kujibia Mtihani na kufaulu.
Mwalimu Miriam Mkama Mkuu wa shule ya Msingi Maendeleo amesema kwa kipindi cha Miaka Saba wamewaandaa kikamilifu kwa kuwapa stadi mbalimbali hivyo anaamini watafaulu kwa kishindo
Kwa upande wake Mwalimu Glory Julius Mabele Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mkuza amesema wanafunzi wote Wana Ari na Moyo wa kufanya Mtihani wa Taifa Mwaka huu kwani wanajiamini kutokana na mazoezi ya vitendo na mitihani ya mara kwa mara waliyopimwa tangu Mwaka 2016 walipoanza darasa la kwanza hivyo amewatakia Mtihani mwema na maandalizi ya kuanza kidato cha kwanza Mwaka 2023.
Haki Zote Zimahifadhiwa