WANANCHI KATA YA MBWAWA NA VISIGA WAPEWA ELIMU YA BIASHARA,NA UMUHIMU WA KODI KWA MAENDELEO,
Wananchi wa Kata ya Mbwawa na Visiga walipata Elimu ya biashara pamoja na mafunzo kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi na kuwajengea uelewa kuhusu mchango wao katika maendeleo ya Taifa .
Katika mafunzo hayo, wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji kibaha walieleza kuwa ulipaji wa kodi ndio msingi wa utekelezaji wa miradi mingi ya kijamii. Wananchi walielezwa kuwa kodi wanazozilipa zimewezesha ujenzi wa shule mpya, upanuzi wa zahanati, uboreshaji wa barabara na Upatikanaji wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya Mbwawa na Visiga.
Viongozi wa Kata Pia walisisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano wa Wananchi katika kulipa kodi kwa hiari, na wakawahimiza kuendeleza moyo huo kwa mustakabali bora wa jamii yao.
Wananchi waliipokea Elimu hiyo kwa shukrani na kueleza kuwa wamepata uelewa mkubwa kuhusu faida za kodi na sasa wako tayari kuwa mabalozi wa mabadiliko kwa kuhimiza ulipaji wa kodi kwa hiari na Uaminifu.
Haki Zote Zimahifadhiwa