Na Byarugaba Innocent,Pwani
Jumla ya Taasisi 552 zinatarajia kushiriki maonyesho ya 29 ya Kanda ya Mashariki ya Nane nane, yatakayofanyika katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere mkoani Morogoro kuanzia Julai 31 hadi Agosti 9 mwaka huu.
Ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo unatarajiwa kufanyika Agosti 2 mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa minne inayounda Kanda ya Mashariki, ofisini kwake Mjini Kibaha Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Abubakari Kunenge alieleza,kati ya Taasisi hizo zilizothibitisha kushiriki ni 372 na zimekamilisha taratibu zote pamoja na maandalizi ya mabanda.
"Kauli mbiu ya maonyesho haya ni Ajenda ya kumi ya thelathini Kilimo ni biashara Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.";
"Ninawakaribisha kushiriki kwenye maonyesho haya ya Nane Nane ambapo
Wilaya 27 zenye Halmashauri 34 zitashiriki na kutakuwa na Teknolojia mbalimbali za kilimo Mifugo na Uvuvi na burudani,"alifafanua Kunenge.
Kunenge alielezea ,litakuwa ni tukio kubwa ambalo litaleta tija kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Kanda ya Mashariki inaunda mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga na wenyeji Morogoro.
Haki Zote Zimahifadhiwa