RAIS MAGUFULI AIMWAGIA SIFA PWANI KWA VIWANDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli yupo Mkoani Pwani kwa ziara ya siku tatu ambapo leo anahitimisha kwa kutembelea Kiwanda Kikubwa cha Uzalishaji wa dawa za kuangamiza Mazalia ya Mbu, Kuweka jiwe la Msingi kwenye kiwanda cha Sayona na kuzindua barabara ya Msata -Bagamoyo.
Mhe. Rais aliyeanza Ziara yake ya Kikazi Juzi Mkoani Pwani alipokelewa na Mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo majira ya saa nane mchana kabla ya kuwahutubia Maelfu wa Wananchi waliofika Kumlaki kwenye viwanja vya Bwawani Mailimoja.
Pamoja na Mambo mengine Mhe. Rais amewataka wananchi kuchapa kazi kwa nguvu zote walizopewa na Mwenyezi Mungu ili kuiondoa Tanzania ilipo kwani nchi hii ni tajiri, yenye vivutio vingi vya kitalii ukiondoa Brazil.
Aidha, Mhe Rais ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Pwani kwa kuweka Mazingira Wezeshi na kuwavutia wawekezaji kwenye sekta ya Viwanda huku akiwataka Wakuu wa Mikoa Mingine Kujiandaa na Majibu siku atakapowauliza sababu za kutokua na viwanda.
Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa, mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Wananchi wa Mkoa wa Pwani wanaunga Mkono kwa vitendo juhudi za Serikali ya Awamu ya tano za kuanzisha Viwanda ili kuinua uchumi wa nchi na kipato chao huku akitoa kilio kwa Mhe.Rais kukosekana kwa umeme wa endelevu na kujengewa barabara zinazounganisha wilaya ya Kisarawe na Bagamoyo kwa Kiwango cha Lami.
Tayari Mhe.Rais ameshazindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye viwanda vya Global packaging kinachotengeneza vifungashio, Kiwanda cha kuunganisha Matrekta aina ya Ursus, Kiwanda cha Kiluwa kinachotengeneza vyuma pamoja na kutembelea Mradi mkubwa wa kuzalisha Maji uliopo Ruvu unaojengwa kwa ufadhiri wa India.
Hii ni ziara ya Kwanza ya Mhe.Rais kuifanya Mkoani Pwani tangu kuchaguliwa kwake Kuingoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2015
Haki Zote Zimahifadhiwa